19th July 2017 21:42:47

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI KWA AJILI YA UHAKIKI WA TUZO MBALIMBALI KWA WALE WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

TAARIFA KWA UMMA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI KWA AJILI YA UHAKIKI WA TUZO MBALIMBALI KWA WALE WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) linapenda kuwafahamisha wahitimu wa Stashahada wanaotaka kujiendeleza katika ngazi ya Shahada kuwa muda wa kufanya maombi ya uhakiki wa tuzo zao umeongezwa hadi tarehe 15 Agosti 2017.

Hivyo kwa wale ambao hawakufanikiwa kumaliza maombi ya uhakiki na wale ambao hawajaomba na wana nia ya kufanya hivyo, sasa wataweza kufanya uhakiki.

Baraza linapenda kutoa rai kwa waombaji kufanya uhakiki wa tuzo zao mapema ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza katika dakika za mwisho wa muda wa uhakiki.

Hakutakuwa na muda wa nyongeza baada ya Tarehe tajwa.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 19/07/2017