18th August 2017 15:15:29

KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI KWA AJILI YA UHAKIKI WA TUZO MBALIMBALI KWA WALE WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

 

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

(NACTE)

 

TAARIFA KWA UMMA

 

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUONGEZWA KWA MUDA WA MAOMBI KWA AJILI YA UHAKIKI WA TUZO MBALIMBALI KWA WALE WANAOKUSUDIA KUOMBA KUJIENDELEZA KATIKA NGAZI YA SHAHADA KATIKA VYUO VYA ELIMU YA JUU KWA MWAKA WA MASOMO 2017/2018

 


Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limepokea maombi ya wadau mbalimbali zikiwemo Taasisi na Vyuo kuhusu kuongezwa kwa muda wa kuhakiki Tuzo za Stashahada kwa wale wanaopenda kujiendeleza katika ngazi ya Shahada katika Vyuo vya Elimu ya Juu.


Hivyo Baraza linapenda kuwafahamisha wadau na wahitimu wa Stashahada wanaotaka kujiendeleza katika ngazi ya Shahada kuwa muda wa kufanya maombi ya uhakiki wa Tuzo zao umeongezwa hadi Tarehe 23 Agosti, 2017.


Hivyo kwa wale ambao hawakufanikiwa kumaliza maombi ya uhakiki na wale ambao hawajaomba na wana nia ya kufanya hivyo, sasa wataweza kufanya uhakiki.


Baraza linapenda kutoa rai kwa waombaji kufanya uhakiki wa Tuzo zao mapema ili kuondoa usumbufu unaoweza kujitokeza katika dakika za mwisho wa muda wa uhakiki.


IMETOLEWA NA:

OFISI YA KATIBU MTENDAJI

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)

TAREHE: 18 Agosti, 2017