UDAHILI AWAMU YA TATU KWA VYUO VYA UALIMU VYA SERIKALI KATIKA PROGRAMU ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA ASTASHAHADA NA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2018/2019

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Simu: 026 2963533, Barua pepe:info@moe.go.tz, Tovuti: www.moe.go.tz

VIGEZO VYA UDAHILI KATIKA PROGRAMU ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA (DIPLOMA) KWA AWAMU YA TATU KWA MWAKA WA MASOMO 2018/2019

VYUO VYA UALIMU VYA SERIKALI

UTANGULIZI

Katika mwaka wa masomo 2018/2019, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itadahili wanachuo 2,943 wa mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada katika Vyuo 9 vya Ualimu vya Serikali kwa masomo ya Sayansi, Sayansi Jamii na Lugha (Kiswahili, ‘English’ na ‘French’,) Hisabati, na Biashara. Hii ni awamu ya tatu ya udahili yenye lengo la kujaza nafasi zilizo wazi.

VIGEZO VYA KUJIUNGA NA NAFASI ZA MAFUNZO BOFYA HAPA